Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenda: Viongozi wa Simba walimkataa Mudathir

Mudathir Yahya Abbas Winner Mwenda: Viongozi wa Simba walimkataa Mudathir

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Yusuph Mwenda amedai kuwa aliwashauri viongozi wa klabu hiyo kumsajili kiungo Mzanzibar, Mudathir Yahya Abbas lakini wakimkataa na leo anakichafua Simba.

Mwenda amedai kuwa viongozi wa Simba wamekuwa wakitaka kusajili wachezaji wenye majina makubwa lakini matokeo yake uwanjani wanakuwa wanafanya vibaya na kuinyima timu ushindi na mataji.

"Wakati Mudathir Yahya anaachana na Azam FC niliambiwa kuna mchezaji anaipenda kweli Simba nikaonana nae alikuwa ni Mudathir Yahya na alionesha dhamira ya kutaka kujiunga na Simba.

"Nikafanya mpango nikampa Ahmed Ally namba ya Mudathir wawasiliane na uongozi Simba walimkataa.

"Wakati mambo yote haya yanafanyika Jimmy Kindoki alikuwepo akamchukua Mudathir viongozi wa Yanga wakampokea na kumpa nafasi mpaka leo anacheza yanga kikosi cha kwanza," amesema Yusuph Mwenda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live