Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwaterema aahidi mabao Dodoma Jiji

Mwaterema Pic Hassan Mwaterema

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji mpya wa Dodoma Jiji, Hassan Mwaterema ameahidi kufunga zaidi mabao kwa msimu ujao akiwa na timu hiyo mpya baada ya kusaini dili la miaka miwili kuitumikia akitokea kwa 'Wanankurukumbi' Kagera Sugar.

Akizungumza Mwaterema alisema atahakikisha anafanya vizuri katika maisha yake mapya kutokana na imani ambayo amepewa na benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo hivyo hayupo tayari kuwaangusha msimu ujao.

"Lengo ni kufanya vizuri kama ambavyo nilifanya nikiwa Kagera Sugar, ninamuomba Mwenyezi Mungu anisaidie niepukane na majeraha tu, kutoka sehemu moja hadi nyingine sio rahisi ila nitapambana kadri ya uwezo wangu". alisema Mwaterema.

Inafahamika kwamba licha ya nyota huyo kutotambulishwa ila amemalizana na walima Zabibu hao wa Dodoma kufuatia mkataba wake na Kagera Sugar kuisha huku wakishindwa kufikia makubaliano ya kandarasi mpya.

Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunatus Johnson aliliambia Mwanaspoti kwamba usajili wao utazingatia matwaka ya benchi la ufundi kwani malengo yao makubwa ni kufanya vizuri zaidi tofauti na msimu uliomalizika Juni 29.

Mbali na Mwaterema ila taarifa zilizopo timu hiyo pia imemalizana na kipa Daniel Mgore aliyekuwa akiitumikia Biashara United na kiungo Jimmy Shoji aliyetoka Mbeya Kwanza ambao timu zao zote zimeshuka daraja msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti