Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanzo wa Ligi, ushindani lazima

Yanga Kmc Dsrs.jpeg Mwanzo wa Ligi, ushindani lazima

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kazi imeanza kwenye anga la kitaifa na kimataifa kwa kila timu kuwa kwenye majukumu yao kutimiza kile ambacho ni muhimu uwanjani.

Msimu mpya unakuwa na mengi mapya kuanzia ratiba pamoja na wachezaji kuwa katika presha ya kufanya vizuri zaidi kuongeza mwendo wa kuwa bora.

Sio Namungo pekee wenye presha ya kufanya vizuri bali Singida Fountain Gate mpaka Geita Gold nao wanahitaji kupata matokeo mazuri.

Malengo ya msimu uliopita ni muhimu kutazama na kujua ni wapi yaligotea kisha kuanza upya pale ambapo yalikwama kwenda sawa ili kuendelea kuwa imara zaidi kwa msimu mwingine.

Iwe kuanzia Championship, Ligi ya Wanawake na Ligi Kuu Bara kila kitu kinapaswa kuwa katika mipangilio mizuri na inawezekana kutokana na muda uliopo kwa wakati huu.

Muda hausubiri kwenye anga la kitaifa na kimataifa vitu vinakwenda kasi na hakuna suala la kusubiri kitakachotokea bali ni lazima kujipanga kwa ajili ya kupata kile ambacho kinatakiwa kwenye kila idara.

Wachezaji ambao watakuwa kwenye changamoto mpya ni lazima kuelewa kuwa wanapaswa kujituma na kuonyesha kile ambacho wengi wanahitaji.

Mwanzo wa ligi tunaona ushindani umekuwa mkubwa hivyo ni muhimu uendelee mpaka mwisho wa ligi hapo tuna amini tutazidi kuwa bora ukizingatia kwamba ligi yetu inazidi kuwa bora.

Kimataifa wameanza kuona picha itakavyokuwa kwenye mechi zijazo na zile ambazo walicheza hii ina maana kuwa kila kona ushindani ni mkubwa na kupata ushindi inawezeka.

Iwe nyumbani ama ugenini kitu cha msingi ni kupambana kwa umakini na kupata matokeo mazuri hilo litaongeza nguvu ya kujiamini na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Mbinu za ushindi zitawapa nguvu ya kusonga mbele hivyo kila mchezo una umuhimu iwe ni nyumbani ama ugenini. Hata ambazo zimepanda ligi ikiwa ni Mashujaa na JKT Tanzania ni muhimu kuleta ushindani.

Kila kitu ili kiwe bora na chenye kuvutia kwenye maisha ya soka kinahitaji maandalizi mazuri hivyo tu basi.

Muhimu kila mmoja kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa umakini na muda uliopo ni sasa hakuna ambaye anapenda kupata matokeo mabaya.

Pia ni muhimu wachezaji kuongeza nidhamu wawapo eneo la mafunzo na wakiwa nje ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza viwango vyao.

Nidhamu ni kitu cha muhimu katika kutimiza majukumu yote na inaongeza uelewa hata pale ambapo mchezaji anakuwa hajaelewa inakuwa rahisi kwa benchi la ufundi kumpa mbinu nyingine Zaidi.

Mashabiki wanapenda kuona matokeo mazuri kwenye mechi zote hivyo wachezaji ni muhimu kuendelea kulitambua hilo na kulifanyia kazi.

Tunatambua kwamba mnajua kuhusu jambo la dakika 90 kuwa na ushindani mkubwa lakini ni muhimu kuendelea kuwa kwenye ubora kila wakati ukizingatia matokeo mazuri ni furaha kwa Watanzania wote.

Kila shabiki anapaswa kuwa pamoja na timu kwenye nyakati zote iwe ni ngumu na zile zenye furaha hii itaongeza nguvu kwa wachezaji kuzidi kupambana zaidi na zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: