Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanzo mwisho sakata la Peter Banda na Ihefu liko hivi

Peter Banda Madeni Peter Banda

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Menejimenti inayomsimamia kiungo raia wa Malawi, Peter Banda imesema inakwenda kwenye kamati ya FIFA kwa ajili ya kuishtaki Klabu ya Singida Black Stars (Ihefu FC) kwa kushindwa kutimiza matakwa ya mkataba wao na mchezaji huyo.

Peter Banda alisaini mkataba wa miaka (2) katika Klabu ya Ihefu Januari 2024 na wala sio Singida Fountain Gate. Gazeti la Malawi lililoripoti halijakosea.

Walikubaliana watampa $ 80,000 kwa ajili ya kusaini mkataba (Signing fee). Banda amesema alilipwa $ 10,000 'Advance' kwa hiyo anaidai klabu ya Ihefu $ 70,000. Ni kweli kaenda kushitaki (FIFA), anadai pesa zake licha ya kwamba hakuwahi kucheza hata mechi moja.

Kwa nini Banda hakucheza?

Imefahamika kuwa, Banda hakucheza kutokana na makosa ya Ihefu wao wenyewe wala sio kosa lake. Jina la Banda halikuingizwa kwenye mfumo wa usajili kwa sababu za kikanuni, Ihefu walikuwa tayari wameingiza majina ya wachezaji 12 wa kigeni kwenye mfumo.

Ihefu na Peter Banda walikaa mezani wakakubaliana Banda aende KMC kwa mkopo, mshahara atalipwa na Ihefu. Zoezi hilo ilishindikana kutokana na gharama za kumhudumia Peter Banda nje ya kambi.

Kwa upande wao KMC walipata mchezaji mwingine wakamsajili wakikimbizana na muda kwani dirisha lilikuwa linakaribia kufungwa.

Dirisha likafungwa akiwa hana timu ikabidi arejee nyumbani kwao Malawi katika klabu ya Nyassa Big Bullets wakati ambao anasubiri dirisha la Tanzania lifunguliwe.

Amesema, tangu hapo Ihefu hawakuwahi kumlipa pesa ya mshahara wala ile Signing fee ya $70,000 iliyobaki.

Msingi wa madai yake Ihefu hHajalipwa mishahara ya Banda kwa miezi (5) hivyo mkataba wake na Ihefu moja kwa moja tayari ulishavunjika kwa kuwa kikanuni inatakiwa isizidi miezi mitatu bila kulipa mshahara wa mchezaji.

Banda anataka alipwe pesa zote za mishahara ya miezi (5) na pesa za signing fee $ 70,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live