Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanzo mbaya kimataifa liwe somo kwa vitendo

Simba, Yanga Waanza Kuweka Viporo Mechi Za NBC Mwanzo mbaya kimataifa liwe somo kwa vitendo

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa kimataifa kwenye mechi za kimataifa nyumbani na ugenini hakuna ambaye ameanza kwa mwendo mzuri.Ipo wazi kuwa ni mwendo mbovu wameanza nao kwa kushindwa kupata matokeo.

Kutokana na kuanza hivyo kwa kushindwa kushinda huku wachezaji wakionekana kutotumia nafasi wanazotengeneza ni muhimu kutumia ubovu huo kuwa darasa huru kwenye mechi zinazofuata.

Yanga na Simba katika mechi za kimataifa za hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kete za Novemba hazijawa na furaha kwao na mashabiki. Simba nyumbani aliambulia pointi moja licha ya kuanza kupata bao la kuongoza.

Yanga wao ugenini walipoteza pointi tatu mazima. Haikuwa wiki nzuri kwa kila upande na matokeo hayakuwa rafiki hasa ukizingatia hesabu zinaanza kupigwa mwanzo.

Ipo wazi kwamba wachezaji wanapenda kuona timu inapata matokeo mazuri hata benchi la ufundi pia mpaka mashabiki. Ikawe hivyo kwa vitendo isiishie kwenye kufikiria tu.

Kwa yote yaliyotokea ni muda wa kufanyia kazi mapungufu kwa wachezaji na benchi la ufundi. Wachezaji mnatakiwa kujituma na kufanya kweli katika kutafuta matokeo.

Bendera ya Tanzania inapeperushwa na wachezaji wote kitaifa na kimataifa. Mechi zijazo kukawe na ari mpya na kasi mpya kwenye kutafuta matokeo uwanjani. Kila la kheri wawakilishi wetu Simba na Yanga kwenye mechi za kimataifa, fanyeni kweli iwe ni nyumbani ama ugenini inawezekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live