Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi mwingine afariki Qatar

Khalid Al Misslam.jpeg Mwandishi mwingine afariki Qatar

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Khalid al-Misslam, Mwandishi wa picha aliyekuwa akifanya kazi na Kituo cha runinga cha Al Kass, amefariki jana huku sababu za kifo chake zikiwa hazifahamiki hadi sasa.

Khalid ni Mwanahabari wa pili kufariki kwenye Kombe la Dunia huko Qatar ikiwa ni saa 48 baada ya Mwanahabari wa Marekani, Grant Wahl kufariki kutokana na shinikizo la damu.

Wahl (48) aliyekuwa akipata shida kuingia Viwanjani kutokana na kuvaa fulana ya kuunga mkono LGBT, alianguka wakati wa muda wa nyongeza katika mechi kati ya Argentina na Uholanzi.

Muda mfupi baada ya kifo cha Wahl, Kaka yake Erik, anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja, alidai kuwa ndugu yake aliuawa kwa sababu ya ukosoaji wake kwa Serikali ya Qatar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live