Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi Rwanda: Uwekezaji wa vilabu Tanzania ni wa kuishia Robo Fainali tu

Clever Kazunguuuuu Mwandishi wa muda mrefu wa habari za michezo nchini Rwanda, Clever Kazungu

Sun, 7 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa muda mrefu wa habari za michezo nchini Rwanda, Clever Kazungu amesema timu za Simba na Yanga kama zinataka kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila kubahatisha basi zinahitaji wachezaji wengi bora kuliko waliopo sasa.

Kazungu amesisitiza kuwa, wachezaji wa kigeni wa Simba na Yanga wengi wao viwango vyao ni vya kawaida na hawana uwezo wa kuzihakikishia klabu hizo kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Uwekezaji wa Simba na Yanga bado ni wa kucheza hatua ya hatua ya makundi na Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tuzipongeze kwa hatua hiyo kwa sababu timu nyingi zinashindwa kufika hapo.”

“Ili kucheza Nusu Fainali, Simba na Yanga bado zinahitaji wachezaji wengi bora zaidi ya waliopo kwa sasa! Hizi timu bado zina wachezaji wengi wa kigeni wenye viwango na uwezo wa kawaida sana ambao hawawezi kukupa uhakika wa Nusu Fainali.”

“Kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika inabidi uwe na wachezaji wa madaraja ya juu. Tanzania timu zinaruhusiwa kusajili wachezaji 12 wa kigeni, lakini kwenye timu unakuta wachezaji watatu au wanne ndio tishio, wengine wa kawaida.”

“Ukiangalia wachezaji wa kigeni wa Simba ni Lakredi, Ngoma, Chama na Che Malone ndio wana ubora wa kuipeleka Simba Nusu Fainali wengine uwezo wao ni wakawaida. Hatua ya Robo Fainali imewasaidia kuona viwango vya wachezaji wao.”

“Yanga imetolewa kwa penati lakini ukiangalia ubora wa wachezaji wa Mamelodi na Yanga unaona kuna tofauti kubwa hata wale ambao wanatokea benchi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live