Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi: Messi alistahili Ballon D'or tano tu, Ronaldo aangua kicheko

OQ TALKSPORT MESSI RON Mwandishi: Messi alistahili Ballon D'or tano tu, Ronaldo aangua kicheko

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Al Nassr FC na Ureno, Cristiano Ronaldo ameacha emoji za kicheko kwenye post ya Instagram ya mwandishi wa habari wa Real Madrid aliyedai Lionel Messi alitakiwa kuwa na Ballon d'Or 5 tu badala ya 8.

Tomas Roncero amesema Ballon d'or kati ya 8 za Messi zilipaswa kwenda kwa Lewandowski, Xavi na Iniesta.

“Ameenda kustaafu huko Miami, lakini alikuwa tayari anaonekana amestaafu alipokwenda PSG kujiandaa na Kombe la Dunia.

Ameshinda Kombe la Dunia, sawa lakini kwa penalti 6 za upendeleo"

"Kombe la Dunia lilifanyika miezi 10 iliyopita na sasa ni Novemba. Messi ana Ballon d'Or nane sawa lakini alipaswa kuwa na tano.

“Ana Ballon d'or za Iniesta/Xavi, Lewandowski ambaye alishinda mataji sita katika msimu mmoja na Haaland ambaye alikuwa mfungaji bora."

Je, unakubaliana na mwandishi huyu wa habari?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live