Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi Afrika Kusini: Mokwena anaiogopa Yanga

MOKWENA Rulani Mokwena, Kocha mkuu wa Mamelodi Sundowns.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa habari kutoka Afrika ya Kusini, Dube Mthoko amesema Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena Hloae anaiogopa Yanga kuelekea mchezo wao wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kati ya Machi 29-30.

"Yanga ni timu kubwa, nilipata bahati ya kuzungumza na kocha Mokwena jioni hii akanambia anaiogopa Yanga, akanambia anaifahamu Yanga vizuri, anafahamu ubora wa Kocha Miguel Gamondi na ameangalia baadhi ya mechi."

"Lakini bado Mamelodi ni moja ya timu bora sana, wamewekeza sana kupitia mmiliki wao Patrice Motsepe, wanaonekana kudhamiria kutaka kushinda taji lao la pili la Ligi ya Mabingwa."

"Kawaida ukiwa unacheza na Mamelodi halafu ukawa unataka kumiliki mpira muda mwingi, utakuwa kwenye hatari sana ya kupoteza mechi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: