Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandembwa ni mwamuzi muoga - Mchambuzi

Emmanuel Mwandembwa.jpeg Mwandembwa ni mwamuzi muoga - Mchambuzi

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka East Afrika Radio, Abissay Stephen amesema kuwa mwamuzi Emmaneul Mwandembwa aliyechezesha mchezo kati ya Coastal Union na Yanga hivi karibuni ni muoga na kwamba anashindwa kufanya maamuzi sahihi awapo uwanjani.

Mwandembwa alishindwa kumpa kadi nyekundu kiungo wa Yanga, Khalid Aucho kwa kosa la kumpiga na kiwiko Ibrahim Ajibu wakati wa mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindoi wa bao 1-0.

"Tukio la Coastal Union Khalid Aucho kumpiga kiwiko Ajibu kaliona na akatoa Yellow, na mchezo ulivyoendelea alishindwa kuumudu, na hii sio mara ya kwanza yeye kufungiwa.

"Hivi sasa kafungiwa miezi 6 kuchezesha mpira, maana yake huyu ameingia kwenye yale makosa ya maonyo, kufungiwa kidogo, kisha akapigwa ndefu kama ilivyokuwa kwa Arajiga.

"Sasa kuna muda unakuta sio Offside lakini unakuta ni faulo ambazo zinaonekana kwa jicho la nyama lakini yeye anaamua kinyume, ni muoga wa kufanya maamuzi, ni sifa hafifu ya mwamuzi wa kati.

"Sasa amekuwa anarudi huyu mtu, swali ni je, nani anampanga?..amekuwa akirudi kwenye kuchezesha michezo licha ya kuwa na rekodi mbaya kabisa ya kuhatarisha maisha ya wachezaji," amesema Abissay Stephen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live