Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasoka wa Iran ahukumiwa kunyongwa

Ng 0789011977.jpeg Mwanasoka wa Iran ahukumiwa kunyongwa

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasoka wa kimataifa wa Iran, Amir Nasr-Azadan amehukumiwa adhabu ya kunyongwa mpaka kufa kutokana na kupigania haki za wanawake na uhuru wa kujieleza nchini mwake.

Nasr-Azadani aliichezea klabu ya Tractor inayoshiriki Ligi ya Iran (Persian Gulf Pro League) kati ya mwaka 2016 mpaka mwaka 2018 na kabla ya hapo aliitumikia Rah Ahan kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Kumekuwa na maandamano nchini Iran tangu mwanamke wa miaka 22 Mahsa Amini afariki akiwa kwenye mikono ya polisi wa maadili nchini humo kwa kile kilichoelezwa hakufuata kanuni sahihi za uvaaji.

Nasr-Azdan ni mmoja kati ya watu watatu waliohudhuria maandamano ya kuipinga serikali na inatajwa kwamba wamelazimishwa kukiri kosa la kuwaua maafisa wa serikali ambapo inatajwa kwamba hakushiriki. Mshambuliaji wa zamani wa Iran, Ali Karimi ametoa wito kwa mamlaka kuondoa adhabu huyo huku mchezaji wa zamani wa Osasuna Masoud Shajaei ameungana na Karimi kupinga adhabu hiyo.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live