Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanariadha Samson Ramadhan awachambua, Failuna, Sarah, Magdalena

97543 MAARATHON+PIC Mwanariadha Samson Ramadhan awachambua, Failuna, Sarah, Magdalena

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Muda mfupi kabla ya wanariadha nyota wa wanawake wa Tanzania, Failuna Abdi, Sarah Ramadhan na Magdalena Shauri kushindana kusaka medali kwenye mbio za Kilimanjaro marathoni, bingwa wa zamani wa jumuiya ya madola, Samson Ramadhan amechambua viwango vya nyota hao huku akitoa nafasi finyu kwa Sarah kufanya vizuri.

Samson ni kocha msaidizi wa wanariadha wa JWTZ ambao wanashindana katika mbio hizo amewapa nafasi ya ushindi Failuna na Magdalena.

"Wakenya ndio washindani wetu, lakini kwa wenyewe kwa wenyewe kwa wanariadha wetu wa kike sioni dalili ya Sarah kufanya vizuri," alisema Samson.

Alisema Sarah licha ya kuwa mgumu  na asiyekubali kushindwa, lakini leo kwenye mbio za Kilimanjaro marathoni hawezi kufanya maajabu.

"Hana mazoezi, nafahamu kwa sababu amekuwa akijifua na sisi, ila kama angekuwa na mazoezi Sarah ni mwanariadha mzuri sana, labda angekimbia mbio za kilomita 21 lakini kwenye full marathoni anajitesa na hatofanya vizuri," alisema.

Upande wa Failuna, Samson alisema kama angekimbia full marathoni naye angejitesa lakini anakimbia mbio za kilomita 21 ambazo ni kama mazoezi kwake.

Pia Soma

Advertisement
"Ana nafasi ya kufanya vizuri kwani kwa mazoezi ambayo amekuwa akifanya hiyo itakuwa kama moja ya mazoezi yake ya kutafuta kasi," alisema.

Upande wa Magdalena ambaye hivi karibuni alivunja rekodi ya Taifa ya nusu marathoni, Samson alisema kama kwenye Kilimanjaro marathoni kungekuwa na mbio za kilomita 10 ndizo zingemfaa zaidi.

"Hata za kilomita 21 anazokimbia si mbaya," alisema Samson.

Chanzo: mwananchi.co.tz