Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwananchi aomba kazi ya kunyonga

Mwqnqnchi 02850 Mwananchi aomba kazi ya kunyonga

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Washiriki wa Mkutano wa haki jinai Kibaha, mkoani Pwani, wamejikuta wanabaki hoi baada ya mmoja wa wakazi mkoani humo, Ramadhani Mauridi, kueleza kuwa anatamani siku moja angeajiriwa na Serikali ili akafanye kazi ya kunyonga watu waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo.

Amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na taarifa zinazoelezwa na vyombo mbalimbali kuwa ni zaidi ya miaka 10 sasa adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi, huku matukio ya mauaji yakiendelea kushamiri nchini hivyo ni vema Serikali ifikie hatua ya kuliangalia hilo ikiwemo hata kuajri watu wenye roho ngumu kama yeye ili waifanye kazi hiyo.

"Haiwezekani mtu anaua kwa makusudi halafu anaenda kukaa gerezani miaka na miaka bila kunyongwa hilo haliwezekani, kama mtu amekutwa na hatia ya kuua naye anyongwe lakini siyo unasikia wengine wanaanza kusema haki za binadamu kwani yeye alipokuwa anaua alikuwa hajui kuwa kuna haki za binadamu? Amehoji mkazi huyo katika mkutano huo uliofanyika Septemba 15, 2023 mjini Kibaha.

Kwa upande wake Hawa John amesema kuwa wakati wajumbe wa haki jinai wakiendelea kufikisha mrejesho kwa jamii juu ya kasoro walizobaini kwenye maswala ya kisheria, suala la baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi kutowalinda watu wanaotoa taarifa za wahalifu linapaswa kuangaliwa ili kulinda usalama wao.

"Kuna baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wanapelekewa taarifa juu ya waharifu, lakini haohao askari wanawaambia waharifu kuwa asingekuwa fulani kutuambia, sisi tusingejua; sasa hilo ni hatari, ni vema sheria iwabane askari wenye tabia hiyo," amesema.

Mjumbe wa tume hiyo, Profesa Edward Hosea, amesema kuwa katika ufuatiliajj wao wamebaini kuwa sheria nyingi zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kulinda haki za wananchi.

"Hata utitiri wa majeshi unapaswa kuangaliwa na kuundiwa sheria upya kwani uwepo wake umekuwa ukileta hofu kwa jamii mfano kuna Jeshi la Zimamoto na Uokoaj na kazi yao kubwa ni kuzima moto, hawa wanapaswa kuwa taasisi tu na siyo kuwa kwenye mfumo wa jeshi," amesema.

Ameongeza kuwa hata majeshi yanayotumika kulinda misitu yasiwe kwenye mfumo wa kutumia silaha kwani hali hiyo inawatia hofu raia.

Mjumbe mwingine wa tume hiyo, Dk Laurean Ndumbaro, amesema kuwa kutosainiwa kwa adhabu ya kifo kwa watu wanaohukumiwa kutumikia adhabu hiyo kwa muda mrefu, kumesababisha uwepo wa mlundikano wa wafungwa wengi magerezani hivyo mapendekezo yao ni kuona utekelezaji huo unaangaliwa upya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live