Mwanahabari Grant Wahl alifariki kutokana na kupasuka kwa mshipa mkubwa moyoni alipokuwa akifanya kazi kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar, amesema mke wake.
Mwanahabari huyo alianguka katika eneo la wanahabari wakati wa Kombe la Dunia wa mechi ya robo fainali ya Argentina na Uholanzi siku ya Ijumaa.
Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 48 alielezea kuhisi shinikizo kifuani mwake siku chache kabla ya mchezo huo.
Mkewe Celine Gounder alisema uchunguzi wa maiti uliofanywa na Ofisi ya Mkaguzi wa Matibabu wa Jiji la New York ulihitimisha kuwa hakuna chochote kibaya katika kifo chake.
"Grant alifariki kutokana na kupasuka kwa mshipa mkubwa moyoni hali inayotokea taratibu na isiyojulikana" alisema Jumatano.
Tatizo hili hutokea pale unapokuwa na uvimbe kwenye mshipa mkubwa wa kwenye moyo ukaziba au hata kupasuka na kusitisha shughuli ya kupeleka damu sehemu zingine za mwilini.
"Shinikizo kwenye kifua alilopata muda mfupi kabla ya kifo chake linaweza kuwa liliwakilisha dalili za awali," aliongeza Gounder, ambaye mwenyewe ni daktari.
"Hakuna kiwango cha CPR au mishtuko ambayo ingemwokoa. Kifo chake hakikuhusiana na Covid. Kifo chake hakikuhusiana na hali yoyote ya chanjo. Hakukuwa na kitu kibaya kuhusu kifo chake."Gounder alishukuru ulimwengu wa michezo kwa heshima kwa marehemu mumewe.
Kifo chake kilisababisha ujumbe kutoka kwa viongozi mbalimbali wa michezo ya Marekani, ikiwa ni pamoja na baadhi ya timu ya Marekani ambayo alikuwa akiicheza nchini Qatar.