Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanachama Yanga ajenga tawi Songwe

Yanga Tawiz Mwanachama Yanga ajenga tawi Songwe

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa Yanga mkoa wa Songwe wameungana kufanya uzinduzi wa tawi jipya la Chimbuya lililojengwa na shabiki mmoja akishirikiana na mwanachama mwenzao aitwaye Godfrey Mwanyombole kutoka Tawi la Tunduma.

Katika uzinduzi huo uliofanyika leo, mgeni rasmi ambaye ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Radwello Mwampashe amewasisitiza wanachama hao kuzingatia maelekezo yanayotolewa na viongozi wao kuanzia ngazi ya taifa.

Naye Mratibu wa Yanga mkoa wa Songwe, Ally Nzowa amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kujisajili na kulipia ada za uanachama.

Licha ya tawi hilo kujengwa na mwanachama mmoja, limekabidhiwa rasmi kwa wanachama wote na kutambulika kama mali ya wanachama wa Yanga mkoa wa Songwe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live