Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MwanaFA atua Misri kuongeza nguvu Taifa Stars

MWANA MwanaFA atua Misri kuongeza nguvu Taifa Stars

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma 'MwanaFA' amesafiri kuelekea nchini Misri kwenda kuongeza nguvu ya hamasa ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda 'Uganda The Crane' unaotarajiwa kupigwa leo Marchi 24, 2024 katika Uwanja wa Ismailia.

MwanaFA amesema, anakwenda huko akimuwakilisha Waziri mwenye dhamana, Dkt Pindi Chana ambaye pia anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

"Mheshimiwa Rais ametoa shilingi milioni 500 kama Stars itafuzu fainali za AFCON sio pesa kidogo, tunamshukuru na tunapaswa kama Watanzania kusimama pamoja kuhakikisha tunafanya kila linalowezekana timu yetu ifuzu," alisema MwanaFA.

Tanzania ipo nafasi ya tatu kwenye Kundi F alama 1 baada ya mechi mbili sawa na Uganda ambayo ipo nafasi ya nne.

Kinara Algeria amefikisha alama 9 kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Niger kwenye mchezo wa raundi ya tatu uliochezwa usiku wa kuamkia leo, huku Niger ikisalia nafasi ya pili ikiwa na alama 2 baada ya mechi tatu.

MSIMAMO KUNDI F #AFCONQ2023

????????³ Algeria: 9 ????????³ Niger: 2 ????????² Tanzania: 1 ????????² Uganda: 1

Chanzo: www.tanzaniaweb.live