Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwana FA: Uwanja wa Maimoria kukarabatiwa

Mwana FA Vsf Mwana FA: Uwanja wa Maimoria kukarabatiwa

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA amesema kuwa Serikali ina mpango wa kuukarabati uwanja wa Maimoria Moshi.

“Kama ambavyo nimejibu mwanzoni viwanja vyote ambavyo vitatumika kwa ajili ya AFCON ujenzi umesha anza na vile ambavyo vitatumika kama sehemu ya mazoezi ujenzi wake utaanza hivi karibuni kwa hiyo mheshimiwa mbunge nimuhakikishie kwa sababu serikali iliahidi kukikarabati kiwaja cha Maimoria Moshi ukarabati huo utaanza hivi karibuni na asiwe na wasiwasi,” amesema Hamis Mwinjuma.

Ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge Ester Maleko ambalo alihoji kuhusu ahadi ya serikali kukarabati uwanja huo ambao utatumika kama uwanjwa wa mazoezi AFCON 2027.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live