Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwana FA: Simba nyakati mbaya zitapita

Mwanafalsafa FA.jpeg Mwana FA: Simba nyakati mbaya zitapita

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, amesema bado ana imani na Kikosi cha Simba kuwa wanao uwezo wa kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika licha ya kupoteza mchezo wa kwanza wa makundi dhidi ya Asec Mimosas.

FA amesema si Simba tu, bali nchi inauhitaji mchezo huu, na amesema matokeo ya hivi karibuni ni kawaida kama ilivyo mambo hanavyotokea kazini, kuna siku zinakuwa nzuri sana, nzuri, nzuri kiasi, kawaida na mbaya.

Ameongeza kuwa wanachopazwa kufahamu ni kwamba zinapokuja nyakati nzuri sana wafahamu kuwa huwa haziwezi kudumu, na hata nyakati mbaya huja na kuondoka na maisha lazima yaendelee!

Je unayo Imani kwamba nyakati nzuri sana walizonazo Yanga zitadumu kwa muda upi na je nyakati chungu kwa Simba zitaondoka lini?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live