Klabu ya Simba imemualika Mhe Hamis Mwinjuma ( Mwana FA) ambaye ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa mgeni rasmi kwenye mechi yao dhidi ya Vipers siku ya Jumanne.
Simba walikuwa na mkutano na waandishi wa habari ambapo kwenye mkutano huo wameongelea mengi ikiwemo ya kuusogeza mchezo kwa masaa matatu mbele badadla ya saa kumi na kupigwa saa moja usiku.
Kupitia Afisa Habari wa klabu hiyo Ahmedy Ally amesema kuwa; “Jumanne yetu tunaita Jumanne ya wenye nchi, lakini pia hauendi kimyakimya, kutakuwa na slogani ya NGUVU MOJA KWA MKAPA HATOKI MTU”
Lakini pia Ahmedy aliongeza kuwa Mwana FA ni mnyama mwenzao lakini Jumanne ataenda uwanjani kama mwakilishi wa Serikali na hawatakuwa tayari kumungusha siku hiyo kubwa kabisa.
Simba kwenye kundi C akiwa na alama tatu wakati kwa upande wa Vipers wao hawajashinda mchezo hata mmoja wakiwa ndio vibonde wa kundi hilo. Mchezo wa Jumanne mnyama anahitaji sana ushindi ili asonge mbele.