Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwana FA: Kung'oa viti Uwanjani ni uhuni

Mwanafalsafaaaaaaa Naibu Waziri, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma "Mwana FA"

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa kung’oa viti uwanjani ni uhuni kama uhuni mwingine na wanaofanya uharibifu huo watachukuliwa hatua.

Ameyasema hayo baada ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya ‘klabu’ ya #Yanga na #Alahly, uliochezwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo baadhi ya wachezaji wa ‘klabu’ ya Yanga wanadaiwa kung’oa viti baada ya mchezo huo ulioisha kwa sare ya bao moja.

Hata hivyo Waziri huyo amewahakikishia Watanzania kuwa waliofanya uharibifu kwenye mchezo huo wa ‘klabu’ bingwa Afrika (CAFL) watachukuliwa hatua kama walivyochukukuliwa hatua waliofanya uharibifu mwaka 2016 kwenye mchezo wa derby kati ya Simba na Yanga nao ulio malizika kwa sare ya 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live