Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi wa kwanza Mwanamke kuchezesha Wembley

Stephanie Frappart Wembley Mwamuzi mwanadada Stephanie Frappart

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi mwanadada Stephanie Frappart ameteuliwa kuwa mwamuzi atakaesimamia mchezo wa kirafiki kati ya England dhidi ya Australia utakaochezwa Oktoba 13, 2023.

Frappart ataweka historia ya kuwa mwamuzi wa kwanza wa kike kusimamia mchezo wa soka la wanaume katika Uwanja wa Wembley.

Mfaransa Frappart alikuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha mchezo wa Kombe la Dunia la wanaume nchini Qatar 2022 alipoongoza ushindi wa 4-2 wa Ujerumani dhidi ya Costa Rica.

Peter Elsworth, mkuu wa waamuzi wa FA, alisema: "Stephanie ni mwamuzi bora. "Tunafuraha yeye na timu yake watachukua jukumu la mchezo wetu ujao dhidi ya Australia mbele ya umati katika Uwanja wa Wembley na tunatazamia kuwakaribisha nyumbani kwa soka la Uingereza."

Frappart ataungana na waamuzi wasaidizi Mikael Berchebru na Aurélien Drouet na afisa wa nne (Fourth official) Hakim Ben El Hadj, huku VAR isimamiwa na Mathieu Vernice, Msaidizi wa VAR atakuwa Nicolas Rainville wote wakiwa ni raia wa Ufaransa.

Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 39 amekuwa mmoja wa waamuzi wa kike, ambao wanasimamia mechi za Ligue 2 na Ligue 1 za wanaume nchini Ufaransa, na pia kuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha Ligi ya Mabingwa na Uefa Super Cup.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live