Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi wa Yanga vs Azam gumzo mitandaoni

Ara 1140x640 Mwamuzi Ahmed Arajiga

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa habari za Michezo Mwandamizi nchini Tanzania Abdul Mkeyenge ameamka na kumlaumu waziwazi Mwamuzi Ahmed Arajiga aliyechezesha mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mabingwa watetezi Young Africans dhidi ya Azam FC, jana Jumanne (Septemba 06).

Miamba hiyo ya Dar es salaam ilikutana Uso kwa Macho Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumbulia matokeo ya sare ya 2-2, huku Mwamuzi Arajiga akigeuka kuwa Gumzo kufuatia maamuzi aliyoyachukua kwa baadhi ya matukio kwenye mchezo huo.

Mkeyenge anaamini Wadau wa Soka la Bongo walikua na nafasi nzuri ya kujadili matukio makubwa ya kiufundi baada ya kuutazama mchezo huo, lakini wameamka na lawama dhidi ya Mwamuzi huyo kutyoka Mkoani Manyara.

Mkeyenge ameandika katika kurasa wake wa Mtandao wa Facebook: “….Mwamuzi ameiharibu sana mechi ya jana iliyokuwa na vitu vingi vya kuvizungumza baada ya kumalizika.”

“Watu hawana tena muda wa kuzungumzia ubora wa Ahmada katika lango la Azam FC.”

“Hawana muda wa kuzungumzia mashuti ya @feisal1994. Hawana muda wa kuzungumzia Kipre JR. Hawana muda wa kumzungumzia Issa Ndala. Kila mmoja, kila mtaa, kila kona, kila kijiwe, kote ni ARAJIGA. ARAJIGA.”

Mwamuzi arajiga analalamikiwa kwa kuruhusu bao la kwanza kusawazisha la Young Africans, ili hali mpira uliozaa bao hilo uliopigwa Beki wa Kushoto Joyce Lomalisa ulikuwa umevuka mstari na kutoka nje.

Tukio lingine analolalamikiwa Mwamuzi huyo ni kuinyima Mkwaju wa Penati Azam FC kufuatia Mshambuliaji Prince Dube kuangushwa eneo la hatari na Bakari Mwamnyeto, huku dakika chache baadae akizawadia Mkwaju wa Penati Young Africans ambayo inadhaniwa Morrison alijiangusha makusudi kwa kumuhadaa Arajiga.

Tukio la Morrison kumkanyaga kwa makusudi beki wa kulia wa Azam FC Lusajo Mwaikenda nalo limechukua nafasi kubwa kwa wadau wa soka la Bongo dhidi ya Mwamuzi Arajiga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live