Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi mechi ya "Derby" apewa somo

Ramadhan KayokopCTSfHPEq5N21 1024x682 Ramadhan Kayoko akiwa katika majukumu yake Uwanjani

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni wazi mwamuzi wa kati siku ya Jumamosi wakati miamba miwili ya Soka Simba na Yanga itakapokutana ni Ramadhani Kayoko.

Hiyo ni baada ya Shirikisho la Soka TFF, kuweka wazi majina ya waamuzi watakaohusika katika mtanange huo.

Ramadhan Kayoko, Kijana mdogo kabisa atasimama kati kati kuhakikisha anawaendesha vigogo hao wa soka la Tanzania.

Kayoko hana mashaka kwa mashabiki wa pande zote hizo mbili, kwani wiki chache zilizopita alishiriki katika matukio makubwa mawili ya Vilabu hivyo Vikongwe nchini.

Kayoko alisimama kama mwamuzi wa kati katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Yanga na Zanaco siku ya kilele cha wiki ya mwananchi ambapo yanga ilipoteza kwa magoli 2-1.

Kayoko huyu huyu alikua mwamuzi wa kati katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa kati ya Simba na TP Mazembe katika kilele cha Tamasha la Simba yaani "Simba Day" ambapo Simba walipoteza mchezo huo kwa goli 1-0.

Katika michezo yote miwili Kayoko alionekana kuimudu vyema presha ya michezo hiyo.

Sasa wadau wa Soka nchin wametoa ushauri kwa mwamuzi huyo kijana mwenye Beji ya uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.

Kuna waliomtaka aache kufoka sana kwa wachezaji kwani anaonekana kuwa mwepesi wa kupandwa na jazba, akiweza kudhibiti hilo basi atakua amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Wadau wamelisemea hilo wakihofu baadhi ya tabia za wachezaji ambao wana mtindo wa kukupandisha ghazabu na kupelekea kufanya makosa. Badala yake atumie zaidi kadi kuonya.

Kwa Upande wa kuchezesha mechi kubwa za ndani Kayoko sio mgeni sana kwani July 12, 2020, alichezesha mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na Simba, simba wakaibuka na ushindi wa goli 4-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live