Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi ashindwa kumaliza mechi Ligi Kuu Zanzibar

Mwamuzi Znz Mwamuzi ashindwa kumaliza mechi Ligi Kuu Zanzibar

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana katika mchezo wa ligi kuu soka visiwani Zanzibar, Mchezo kati ya KVZ dhidi ya Kundemba FC uliochezwa katika uwanja wa Mau majira ya saa 10:15 jioni ulishuhudiwa hali isiyo ya kawaida baada ya mwamuzi wa mchezo huo Hamiar Abdallah Muhsin kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kuanguka ghafla kiwanjani dakika ya 70 ya mchezo

Mchezo huo kwa dakika 20 zilizobaki ulichezeshwa na mwamuzi wa akiba Nassir Salum Siyai.

Madaktari walipoingia uwanjani walieleza kua kijana huyo amekumbwa na kizunguzungu.

Aidha baadae Madaktari walieleza kua Hamiar anasumbuliwa na misuli kubana jambo ambayo limesababishwa na mazoezi magumu na ya muda mrefu yanayofanywa na waamuzi hao hususan siku za mechi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live