Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi anaedaiwa kumpiga kiwiko Robertson awekwa mtu kati

D2965BF2 3BC0 4979 A2F8 C728BA4EDC19.jpeg Mwamuzi aliempiga kiwiko Robertson hatarini kukumbana na adhabu

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachambuzi wa soka wameshinikiza mwamuzi wa msadizi afungiwe baada ya kumpiga kiwiko nyota wa Liverpool, Andy Robertson kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal uliyochezwa wikiendi iliyopita.

Liverpool na Arsenal zilitoka sare ya mabao 2-2 baada ya Mohamed na Roberto Firmino kusawazisha baada ya Gabriel Martinelli na Gabriel Jesus kucheka na nyavu.

Lakini mwamuzi huyo Constantine Hatzidakis aliteka vichwa vya habari wakati wa mapumziko kutokana na sintofahamu iliyotokea kati yake na Robertson.

Video ilimuonyesha Hatzidakis akijibizana maneno na Robertson kabla ya kumpiga kiwiko kitendo ambacho kilizua gumzo mtandaoni na kulaaniwa na wadau wa soka.

Chama cha waamuzi England (PGMOL) kitangaza kwamba uchunguzi utafanyika kutokana na tukio hilo lilitokea kwenye mchezo huo wa ligi.

Aidha wachumbuzi wa soka maarufu akiwemo Darrent Bent alisisitiza mwamuzi huyo afungiwe zaidi ya mechi nane kutokana kitendo chake cha kumpiga kiwiko beki wa Liverpool: "Haiwezekani mwamuzi afungiwe mechi nane kama mchezaji wa Fulham, Aleksandar Mitrovic," alindika kupitia akaunti yake ya twitter

Ikumbukwe Mitrovic alifungiwa mechi nane na bodi baada ya kumsukuma refa Chris Kavanagh kwenye mechi yao ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United, mwezi uliopita.

Naye straika wa zamani wa aliyewahi kukiwasha Ligi Kuu England, Chris Sutton alisema "matukio kama hayo hayakubaliki kwenye soka, kwahiyo mwamuzi huyo apewe adhabu haraka iwezekenavyo" kauli hiyo alizungumza kupitia kituo cha televisheni cha BBC.

Bodi ya waamuzi ilitoa tamko rasmi ikidaiwa kwamba wanatambua tukio hilo lililotokea kwenye mechi ya ligi kati ya Liverpool na Arsenal ambao ulichezwa uwanja wa Anfield, kwahiyo uongozi utafuatilia kwa makini kabla ya kutoa adhabu yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live