Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi aliemaliza mpira kabla ya dakika 90' astaafu

Sikazweee Mwamuzi Janny Sikazwe

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi wa Kati, Janny Sikazwe, ametangaza kustaafu kuchezesha soka, baada ya kuhusika katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Sikazwe (43) raia wa Zambia kama utamkumbuka vema kwenye sakata la kumaliza mechi mara mbili kabla ya muda (90') kufika, alichezesha ya Tunisia dhidi ya Mali na alimaliza mchezo huo dakika ya 85' na baadae tena uliendelea na alimaliza tena dakika ya 89' yaani haikufika tena dakika 90'.

Mwamuzi amefichua kwamba alikaribia kufa wakati wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyofanyika nchini Cameroon na anasema ilikuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake.

"Nilikaribia kufa (nilipomaliza Mechi mapema kwa sababu ya joto kali) kwenye AFCON ya 2021. Ilikuwa mechi mbaya zaidi ya kazi yangu."

Sikazwe amesema, anafuraha kustaafu kama mwamuzi wa Zambia aliyefanikiwa zaidi katika historia.

Janny Sikazwe alikuwa mmoja wa waamuzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 205, Alichezesha Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA 2016 Japan.

Februari,5, 2017 alichezesha Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon ambayo ilishuhudia Cameroon wakiibuka Mabingwa wa Afrika baada ya bao la dakika ya 89 Vincent Aboubakar lililowafanya kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Misri.

Juni, 18, 2018 alikuwa mwamuzi wa kwanza wa Zambia kuchezesha mchezo katika fainali za Kombe la Dunia la FIFA.

Januari, 12, 2022 alichezesha Kombe la Mataifa ya Afrika 2021, katika mchezo wa Kundi F kati ya Mali na Tunisia.

Novemba, 23 mwaka huu alichezesha Kombe la Dunia 2022, katika mchezo wa Kundi F kati ya Ubelgiji na Canada ambao ulishuhudia Ubelgiji wakiibuka washindi kwa bao 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live