Klabu ya Al Ahly imeweka historia baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ta 11.
Naweza kusema kuwa ni Ubingwa ambao timu hiyo imeusotea sana naada ya kupitia wakati mgumu katika hatua ya makundi.
Ikumbukwe kuwa Al Ahly ilipigana kufa na kupona ili kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindani hayo ikipitia mfupa mgumu wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal Omdurman ya Sudani na Coton Sport ya Cameroon.
Mamelodi Sundowns ilimaliza ya kwanza katika kundi B kwa kukusanya jumla ya pointi 14 na kufuatiwa na timu ya Al Ahly iukiwa na pointi 10 sawa na Al Hilal huku Coton Sport ikiwa ya mwisho kwa kutokuwa na pointi. Ni wastani wa mabo ya kufunga na kufungwa tu ndiyo iliyoikoa timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali.
Katika hatua ya robo fainali, Al Ahly ilifanikiwa kuitoa Raja Cassablanca kwa mabao 2-0 na baadaye kuitoa Esperance ya Tunisia kwa idadi ya mabao 3-1 na baadaye kufushinda taji la Afrika kwa idadi ya mabao 3-2 dhidi ya waliokuwa Mabingwa watetezi Wydad Club Athletic.
Ni ubingwa ambao klabu hiyo haitausahau kutokana na safari iliyokuwa na mabonde mengi na milima ambayo ilikuwa na vikwazo vingi.
Nimeanza kuwapa historia hiyo ya Al Ahly ili kuweka sawa kwani mechi ya mwisho dhidi ya Wydad ilichezeshwa na mwamuzi Bamlak Tessema Weyesa aliyezaliwa Desemba 30 mwaka 1982.
Ni mwamuzi msomi na pia anafanya kazi katika chuo kikuu cha Addis Ababa ambapo alihitimu digrii yake ya ‘socology’ mwaka 2012. Kubwa kwa mwamuzi huyo ni kuwa mechi hiyo ya fainali ilikuwa ya mwisho kwake kwani aikuwa ana-stahafu.
Kuona hvyo, CAF ilimpa heshima kubwa kuchezesha mechi hiyo ya fainali ili kumuaga rasmi pamoja na vipingamizi kutoka kwa kocha wa Al Ahly Marcel Kollerambaye akikosoa na kupinga uteuzi huo.
"Kumtaja Bamlak Tessema kuchezesha mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Wydad ni jambo la kuudhi na linalotia wasiwasi sana kwani utakuwa mchezo wake wa mwisho na atastaafu baada ya hapo," alisema Koller.
"Mwamuzi hatakuwa na ahadi au majukumu yoyote baada ya mchezo. "Tunatumai atatushangaza kwa uamuzi wa haki."
Kocha huyo alisema kuwa katika mchezo wa kwanza alishuhudia maamuzi kadhaa yenye utata ya waamuzi ambayo Koller alidai yalikuwa na athari kubwa kwenye mchezo.
Alisema kuwa VAR iliingilia kati na kubatilisha uamuzi wa adhabu kwa Ahly, huku dai la penalti ya faida kwa timu yake likikataliwa pamoja na rufaa ya kadi nyekundu kwa kunyima nafasi ya wazi pia ilikataliwa.
Mchezo huo wa kwanza ulichezeshwa na mwamuzi Motaz Ibrahim ambaye alikabiliwa na pingamizi kubwa kutoka kwa wachezaji wa Ahly wakati beki wa mwisho, Yahia Attiat Allah, alipoumiliki mpira kimakusudi kuwazuia Percy Tau na Hussein El Shahat kusonga mbele kuelekea langoni huku matokeo yakiwa bado 2-0. Hata hivyo, mwamuzi wa Libya alitoa kadi ya njano pekee. Koller alikiri kwamba alikasirishwa na matokeo licha ya kupata ushindi.
Tessema, 43, amechezesha michezo 38 katika Ligi ya Mabingwa ya CAF tangu aanze kucheza msimu wa 2012/13.
Mwamuzi huyo amechezesha fainali mbili za Ligi ya Mabingwa katika maisha yake ya soka, huku Ahly wakiishia kuwa timu iliyopoteza mara zote mbili.
TESSEMA ALIVYOMKOA KOLLER NA KUUPIGA MWINGI
Kinyume na mawazo hasi ya kocha wa Al Ahly, Tessema ailionyesha jinsi gani mwamuzi wa kati anavyotakiwa kufanya majukumu yake kwa mujibu wa sheria za soka duniani.
Mwamuzi huyo alichezesha kwa ustadi mkubwa mechi hiyo iliyojaa kila aina ya vitimbi kutoka kwa wachezaji wa timu zote mbili. Hakupendelea na kila kwenye tukio, alifanikiwa kufika na kutoa maamuzi ya haki.
Cha kushangaza zaidi, hakuwa tayari kutumia teknolojia ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) na kutoa ‘somo’ kwa waamuzi waliobaki.
Ameonyesha kuwa VAR ni teknolojia ya ziada kwake na kwa mwamuzi ambaye anajali fani yake, hawezi kuitumia kamwe.
Kwa kocha Koller, amebaki kuwa na somo kubwa dhidi yake. Kwani Tessema amemuachia ‘homework’ ambayo mbali ya kusheherekea ubingwa, atakuwa anafikiria zaidi mwamuzi ambaye aliyempinga kabla, na kuumbuka baadaye.