Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto yuko fiti kuwavaa Prisons Mbeya

Mwamnyeto 0474 Bakari Nondo Mwamnyeto

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuwa nje kwa takriban michezo miwili ya Ligi kwa sababu ya Majeraha, Nahodha na mlinzi wa Yanga Bakari Mwamnyeto amejiunga na timu kuelekea Jijini Mbeya tayari

“Tunategemea urejeo wa Bakari Nondo Mwamnyeto katika kikosi baada ya kurejea akiwa na majeraha akitokea katika timu ya taifa kwenye michuano ya AFCON, hivyo anarejea katika kikosi na atakuwa kwenye safari ya kuelekea Mbeya.

“Tunategemea kuwakosa baadhi ya wachezaji ambao wanaweza wakawa wamepata majeraha kwenye mchezo wa juzi na itategemea na ripoti ya daktari mpaka pale ambapo tutakuwa tunasafiri, kwa maana ya Ibrahim Abdullah (Bacca) pamoja na Gift Fred, hao ndio wachezaji ambao mpaka muda wa kusafiri tutakuwa tumeshajua hali zao na kujua kama wataambatana na timu au la, lakini kwa wengine wote watakuwa tayari kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kikosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: