Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto hajaisha, lakini kilichopo Yanga ni hiki!

Mwamnyeto Zmsh Mwamnyeto hajaisha, lakini kilichopo Yanga ni hiki!

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlitazama Captain Bakari Nondo Mwamnyeto jana? Achana na penati ambayo aliipiga ya uhakika ila rejea mechi zote dume za Yanga ama nyakati zote ngumu Muungwana kutoka Tanga huwa anakuonesha kitu, nimefanya tafiti zangu nimegundua watu kutoka TANGA wana roho ngumu mno, imagine kelele zote za Wananchi wengi kutokuwa na imani nae anaenda kupiga tuta gumu mno pale Amani.

Itazame vyema sana hii picha, usimtazame kapteni Nondo bali watazame Wachezaji nyuma yake (background) watazame vizuri kabisa kwa kutulia, nadhani umegundua kitu! Umeona tabasamu zao wanavyomtazama Kiongozi wao? Umeona walivyotulia bila kusogea kumghasi? Umeona wanavyomtazama kwa mahaba? Hii ndio maana ya kuvaa kitambaa na kusimama kama Kiongozi.

Kafuatilie mechi vyema wakati wa hili tukio, walitulia wote na Captain akamaliza kufanya vyote alivyotaka, kumbuka nyuma yake kuna Mastaa kibao pengine kumzidi ila wao wanamtambua kama Kiongozi wao, hapa unajifunza kitu kingine! Standard aliyojiwekea na hali ya nidhamu kwenye timu, hakuna aliye juu ya mwingine bali utaratibu pekee.

Hii ndio maana Azam walikuwa wa kwanza kutuma ofa kwa Uongozi wa Bakari, walimtaka ila Meneja wake ambaye ni Shemeji yake Kassa Mussa aliwaambia haiwezekani, hii ndio maana hata Simba wanamtaka sana, unahitaji talent kama yake, Uongozi kama wake yani sauti ya mamlaka kuamrisha wengine.

Sitaki kuamini kama Nondo ameisha ila football ilivyo, Bacca na Job wana maelewano mazuri na wapo kwenye kiwango bora sana, ni kawaida kwenye football.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live