Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto awaita Wananchi Dodoma

Mashabiki Wa Yangaa Mashabiki wa Yanga

Wed, 10 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha ya Young Africans SC, kipo jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB Bank ambayo hapo awali ilikuwa ikifahamika kama Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Mchezo huo wa hatua ya 16 bora, unatarajiwa kupigwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuanzia saa 2:00 usiku.

Nahodha wa Young Africans SC, Bakari Mwamnyeto, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti katika mchezo huo.

“Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kutusapoti kwani hii ni timu yao na sisi tupo tayari kuipambania timu kufikia malengo ya kutetea ubingwa wetu,” alisema Mwamnyeto.

Ikumbukwe kwamba, Young Africans SC ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo ikishinda taji hilo mara mbili mfululizo msimu wa 2022-2022 na 2022-2023.

Itakumbukwa kuwa, jana mahasimu wao Simba SC waliondoshwa kwenye michuano hiyo na Mashujaa FC ya Kigoma kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoa sare ya bao 1-1 mdani ya dakika 90.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live