Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto awaita Wananchi

Yangaaa Kombe Mwamnyeto awaita Wananchi

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa kikosi cha Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto, amewaomba mashabiki wa Young Africans popote walipo, kujitokeza kwa wingi Jumapili katika fainali ya Kombe la CRDB Bank dhidi ya Azam.

Mchezo huo utachezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku ambapo Young Africans wataingia wqkiwa mabingwa watetezi.

“Tunashukuru Mwenyezi Mungu tumefika salama na tumeanza maandalizi ya fainali, vijana wapo tayari kwenda kulitetea Kombe la CRDB.

“Mpaka sasa umeona mchango wa wakongwe ni wa hali ya juu kwa vijana na tayari tumeinua kwapa (ubingwa wa ligi kuu) na Inshaallah tunakwenda kunyanyua tena Jumapili.

“Wewe Mwananchi wa Zanzibar, wewe shabiki wa Young Africans tupo kwako Zanzibar, nawaombea Mungu wanaotokea Dar es Salaam na mikoa mingine kuja kuangalia hii fainali tuwaambie tu Amaan siku ya fainali basi iwe kijani na njano, nina imani tutatetea tena ubingwa wetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live