Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto ataka rekodi Yanga

Mwamnyeto 10 Milioni Mwamnyeto ataka rekodi Yanga

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutwaa mataji mawili ya ligi mara mbili mfululizo, nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema anafurahi kuongoza timu yenye mafanikio sasa anapambana kuandika rekodi yake mwenyewe ndani ya timu hiyo.

Mwamnyeto alitua Yanga akitokea Coastal Union ametwaa mataji matatu akiwa na timu hiyo hadi sasa akianza na Ligi kuu msimu uliopita na Ngao ya jamii na msimu huu amewaongoza mastaa wenzake kutwaa taji la pili la ligi.

Akizungumza nasi, Mwamnyeto alisema anafurahi kuwa miongoni mwa mastaa ambao wanatarajia kunyanyua kwapa kwa mara nyingine baada ya kutwaa taji la ligi lakini ndoto yake kubwa ni ubingwa wa Afrika.

"Kutwaa taji la ligi ni furaha lakini sio rekodi kubwa kwasababu ni manahodha wengi wametwaa mataji hayo ambayo hadi sasa wanayo 29 natamani kuwa nahiodha wa kwanza mwenye mafanikio makubwa ndani ya Yanga;

"Kwa kuwaongoza wachezaji wenzangu ambao kwa asilimia kubwa wanauchu wa mafanijkio kuhakikisha tinatwaa taji la Afrika la Kombe la Shirikisho hii ndio itakuwa rekodi yangu kubwa kwenye maisha yangu ya soka."

Mwamnyeto alisema hatua waliyofikia kutinga nusu fainali sio haba lakini anatamani kuandika historia kwa kutwaa kabisa taji la mashindano hayo makubwa huku akiwaahidi mashabiki kwenda kupambana dhidi ya Marumo ili watinge fainali.

"Tuna mchezo mgumu wa marudiano dhidi ya Marumo fulaha ya ubingwa tunaiweka pembeni tunazingatia mchezo ulio mbele yetu tutaingia tukiwa na morali ya kutosha lengo ni kufikia lengo la kucheza fainali na hatimaye kutwaa taji;

"Ni furaha kuongoza wachezaji ambao wanakupa ushirikiano mzuri uwanjani na wana uchu wa mafanikio naiona Yanga ikifikia malengo ya kucheza fainali kutokana na namna wachezaji na benchi la ufundi wanavyochukulia umuhimu wa mchezo ulio mbele yetu," alisema Mwamnyeto.

Akizungumzia msimu wa 2022/23 alisema ulikuwa ni msimu bora kwao pamoja na kushindwa kuvunja rekodi yao wawo wenyewe ya kutwaa taji bila kufungwa wanashukuru wameweza kulitetea taji na wanaamini utakuwa ni msimu wao bora zaidi wakifika fainali na kutwaa taji la Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: