Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto ataja siri ya kuwachapa Simba 5-1

Mwamnyeto 0474 Mwamnyeto ataja siri ya kuwachapa Simba 5-1

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki na kapteni wa Yanga SC, Bakari Mwamnyeto ametaja siri iliyowafanya waweze kuibuka na ushindi wa goli 5-1 dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC.

Akiuzungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar jana Novemba 5, 2023, Mwamnyeto alisema, baada ya kupata goli la kuongoza na kisha Simba kusawazisha, alizungumza na wachezaji wake kuwaambia watulie.

"Niliwaambia watulie, tusiwavamie kwanza sababu Simba ni timu kubwa, tunatakiwa tuliandi kwanza huku tukishambulia kwa tahadhali," alisema Mwamnyeto.

Kwa ushindi huo mzito, Yanga amezidi kujikita kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na alama zake 21 baada ya kucheza michezo 8 huku Simba wakishika nafasi 3 wakiwa na alama 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live