Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto ashusha presha Yanga

MWAMNYETO2 Mwamnyeto ashusha presha Yanga

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NAHODHA Mkuu wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amesema kuwa malengo yao katika msimu huu ni kubeba mataji yote katika msimu huu huku nguvu na akili wakizielekeza katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya Simba kufanikiwa kufuzu Robo Fainali ya FA kwa kuwafunga Ruvu Shooting mabao 7-0, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Jumanne.

Yanga wanacheza na Mtibwa Sugar Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Mwamnyeto alisema kuwa mara baada ya kushinda mchezo wao wa Biashara na kufuzu hatua ya Robo Fainali ya FA, hivi sasa nguvu zao wanazielekeza katika mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa.

“Niwaombe mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuisapoti timu yao ili tufanikishe malengo yetu katika msimu huu ambayo ni kuchukua makombe yote tutakayoshindania.

“Sisi kama wachezaji tutafanya kila linalowezekana kuwapa furaha na kufanikisha malengo yetu tuliyoyapanga mwanzoni mwa msimu huu ambayo ni kuchukua makombe yote.

“Hivyo aliyepo mbele yetu ajipange vizuri yule tutakayekutana katika ligi au FA, mashabiki wafahamu kuwa sisi wachezaji wao tutapambana kila tutakapokuwepo uwanjani kufanikisha ushindi ili wapate furaha,” alisema Mwamnyeto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live