Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto apewa mchongo Yanga

Mwamnyeto Pic Data.png Mwamnyeto apewa mchongo Yanga

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amepewa mchongo mpya wa kurejea kwenye kiwango chake, ili kuwaondoa wasiwasi mashabiki wanamuona ameshuka na pengine kuja kuiyumbisha safu ya timu yao ambayo tangu msimu uanze amekuwa akicheza kikosi cha kwanza sambamba na Lamine Moro.

Mwamnyeto alisajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Coastal Union, huku akiwa imara na Lamine ndani ya timu yao, ingawa hivi karibuni ameonekana anatoa maboko yaliyowafanya wachambuzi kumjadili na kumpa mbinu za kurejea kwenye mstari.

Mchambuzi maarufu wa soka nchini, Mwalimu Alex Kashasha, alisema hashangazwi na kiwango cha Mwamnyeto kushuka tofauti na alivyoanza msimu, kwamba inawezekana ikawa uchovu wa kucheza mechi nyingi pamoja na tatizo la kuondokewa na mke na mtoto, analoliona linatakiwa apate watu wakumjenga ili aendelee kutoa huduma yake ndani ya kikosi hicho.

“Ni kweli kila mmoja ana jicho lake la kuona kiwango cha mchezaji, binafsi namuona mbali endapo akizingatia miiko ya soka ndani ya uwanja kwa kutoishiwa maarifa, pia kujitunza mwili wake nje ya uwanja, huwa namkubali sana Erasto Nyoni kwa namna ambavyo muda wote akicheza unamuona ana kitu kipya, hachoshi kumtazama, liwe funzo kwa wadogo zake,” alisema Kashasha na kuongeza;

“Wakati mwingine mchezaji akifanya mazoezi magumu sana, akifika uwanjani anakuwa anaona hakuna jambo jipya, ukiondoa hilo tusisahau alitoka kupata pigo kubwa la kufiwa na mke na mtoto.

“Benchi la ufundi na viongozi wamjenge na pia kumsahihisha baadhi ya makosa madogomadogo anayoyafanya, akiendelea kukomaa mengine atakuja kujirekebisha mwenyewe, ila bado ni mzuri kwa Stars na Yanga klabu yake,” alisema.

Naye staa wa zamani wa Mecco ya Mbeya, Abeid Kasabalala alisema kuna vipindi viwili kwa mchezaji, kiwango kuwa juu na kiwango kushuka, lakini itategemeana na nidhamu yake ya namna ya kuheshimu nyakati hizo ili kulinda bora na kipaji chake kwa muda wote.

“Kama shida ni uchovu wa kucheza mechi nyingi, anatakiwa awe na nidhamu ya kujitunza ndani na nje ya uwanja, hilo litamsaidia asitoke nje ya mstari, lakini pia bado ni kijana mdogo anayetakiwa kuweka malengo ya kufika mbali, asiridhike na kuona ameishamaliza kucheza Yanga.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz