Bakari Nondo Mwamnyeto amewahi kupita kwenye kipindi kigumu zaidi ya hiki msimu uliyopita, kiasi alipoteza nafasi ya kwanza kwenye kikosi chini ya Prof Nasreddine Nabi.
Lakin alitambua hilo na kurejea kwenye uwanja wa mazoezi na kuongeza juhudi na kusahihisha makosa yake na hatimaye alianza kurejea kwenye kikosi na kufanya vyema sana.
Hizi ndizo hatua wachezaji wakubwa hufanya endapo huwa kwenye kipindi cha mpito.
Nilipoona taarifa za kwamba kagoma kurejea Kikosini kisa ufinyu wa nafasi kidg ilinipa mashaka lakin lisemwalo lipo na kama halipo laja ndivyo waswahili husema lakin nkasubir kuona kama kweli hatorejea kwenye kikosi.
Lakin tayari yupo kikosini na anaendelea na majukumu yake na timu yake ya Yanga Sc, ni wazi hata kama Taarifa hizo ni kweli lakin siamin kama Naodha kama Bakari anaweza kutumia njia hiyo kudai nafasi kwenye kikosi, zipo njia ambazo anaweza kutumia kufanya hivyo ila kugoma kurudi kikosini sidhani kama naweza amini katika hilo na mwamnyeto ni mtu mwenye busara sana hawez kutumia njia kama hizo.
Ukizingatia ndiye nahodha hawez kuwa mfano mbaya na hii inaweza kuwa one of the worst thing in football. Msingi amesharejea kwenye kikosi sina budi kusema kuzipuuzia zile tetesi.