Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto aahidi makubwa Tunisia

Mwamnyeto Na Moloko 1140x640 Beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto na Jesus Moloko

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: dar24.com

Beki na Nahodha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Bakari Nondo Mwamnyeto ameahidi watapambana kwenye mchezo wa Mkondo wa Pili Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Hatua ya Mtoano dhidi ya Club Africain.

Young Africans itacheza ugenini Tunis-Tunisia keshokutwa Jumatano (Novemba 09), ikiwa na deni la kufuzu Hatua ya Makundi, baada ya kuambulia sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Novemba 02.

Mwamnyeto amesema wanatambua wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo dhidi ya Club Africain, hivyo hawana budi kupambana hadi kufikia lengo la kufuzu Hatua ya Makundi kwa kupata ushindi ugenini.

Hata hivyo Beki huyo amewataka Watanzania wenye mapenzi na Young Africans kuungana kwa pamoja na kuiombea timu yao, ili ifanikishe lengo lililowapeleka nchini Tunisia.

“Tuna dakika 90 ngumu, subirini muone, kwa sababu wachezaji tumejipanga kufanya kilicho bora. Ni mchezo muhimu kwa kila upande, ninaamini kila mmoja amejiandaa,”

“Kwa upande wa Viongozi na Benchi la ufundi wamemaliza mambo yote, kazi imebaki kwetu sisi wachezaji kwenda kupambana ndani ya uwanja na kuzimaliza dakika 90 kama vita ya mapigano makubwa.”

“Tunaomba ushirikiano kutoka kwa Mashabiki wa wote Tanzania wenye mapenzi na timu yetu, ninaamini nafasi ya kusonga mbele tunayo, ni suala la muda tu kila kitu kinawezekana kama wao waliweza kutuzuia nyumbani, basi na sisi tunapaswa kufanya hivyo na kushinda huumchezo.” amesema Mwamnyeto

Young Africans inatakiwa kushinda ama kupata sare yoyote ya mabao ili kufanikisha safari ya kucheza Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Msimu huu 2022/23.

Chanzo: dar24.com