Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto: Yanga Tunabeba Ubingwa ASFC

Beki Yanga Mwamnyeto: Yanga Tunabeba Ubingwa ASFC

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BEKI wa kati wa Yanga ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto, amesema safari hii wanahitaji kufika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kuwa mabingwa.

Yanga juzi Jumanne walifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mwamnyeto alisema, malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa michuano hiyo.

“Tunatakiwa kufika fainali ili tuwe mabingwa wa a michuano hii, akili zetu na malengo yetu yapo katika michuano hii na lazima tuhakikishe tunatimiza.

“Wapinzani wanatakiwa kujipanga kwani hata sisi tayari tumeshajipanga kucheza na timu yoyote itakayojitokeza mbele yetu, hakuna jambo ambalo lisilowezekana, ni kujituma tu na kuwa na nia ya kuwa mabingwa na sisi tunayo nia,” alisema nahodha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live