Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto: Tutajitoa kwa hali na mali

Mwamnyeto 0474 Bakari Mwamnyeto

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Klabu ya Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto amesema kuwa wao kama wachezaji watajitoa kwa hali na mali lwenye mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns kuhakikisha wanapata ushindi ili kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano ya CAFCL.

Yanga watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Mamelodi kesho nchini Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya CAFCL baada ya mchezo wa walai kutoka sare ya bila kufungana katika Dimba la Mkapa.

"Wachezaji na benchi la ufundi tunawaombea Wanachama na Mashabiki wetu wanaosafiri umbali mrefu kutoka Tanzania kuja hapa Afrika Kusini kutusapoti wafike salama na sisi tutajitoa kwa hali na mali kuhakikisha tunaondoka na ushindi," amesema Mwamnyeto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live