Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto: Penati ya Pacome ilifufua matumaini yetu

Yanga Pc Crdb Mwamnyeto: Penati ya Pacome ilifufua matumaini yetu

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Klabu ya Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto amesema kuwa anajivunia kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kombe la shirikisho mara tatu mfululizo akiwa kama kapteni wa miamba hao wa soka Tanzania.

Mwamnyeto amesema hayo baada ya kuibuka mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB kwa kuwafunga Azam Fc kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5 baada ya kutoka sare dakika 120 za kucheza.

Aidha, Mwamnyeto amesema kuwa penati ya tatu iliyopigwa na Pacome Zouzoua iliamsha matumaini kwa wachezaji na benchi la ufundi hasa ikikumbukwa kuwa tayari walikuwa wamepoteza penati 2 za mwanzo na Azam wakipata penati 2 za mwanzo.

"Najivunia kuchukua kombe mara tatu ndani ya Yanga SC kama Nahodha ni furaha kubwa na historia nzuri na tunawashukuru mashabiki wasikate tamaa hii ndio timu yao na kuhusu kuondoka msimu umemaliza ngoja tuone.

“Hii ni fainali na fainali ina ugumu wake, timu zote ni nzuri na wachezaji tunajuana na kizuri zaidi tumekutana kwenye mechi mbalimbali, kwa hiyo kila mmoja alijipanga kuchukua ubingwa lakini bahati nzuri ikawa kwetu tumeshinda kwa mikwaju ya penati.

“Mpaka mtu ananyanyuliwa kwenda kupiga penati maana yake mwalimu anamuamini na mimi ninajiamini nimekwenda kupiga penati nisimwangushe mwalimu.

“Baada ya wenzetu wawili kukosa penati za mwanzo (Aziz Ki na Guede, penati ya Pacome ilifufua matumaini ma morali kwa wachezaji wote na wao Azam wakaanza kupata woga, hicho ndicho kimetusaidia tukashinda," amesema Mwamnyeto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live