Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto: Ndoto zimetimia Ligi ya CAF

Mzize Yanga Konkoni Skudu Mwamnyeto Mwamnyeto: Ndoto zimetimia Ligi ya CAF

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Yanga, Bakar Mwamnyeto amesema kitendo cha timu hiyo kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupita miaka 25, imemfanya aingie kwenye historia ya klabu hiyo akisema ndoto zimetimia kwani kila mchezaji alikuwa anaumizwa na kelele za kushindwa kutinga hatua hiyo.

Yanga ikicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam juzi iliifunga Al Merrikh ya Sudan na kuitoa kwa jumla ya mabao 3-0, kwani mchezo wa kwanza wa ugenini timu hiyo ilishinda mabao 2-0 jijini Kigali, Rwanda na kutinga makundi tangu ilipofuzu mara ya mwisho mwaka 1998.

Kitendo cha kuwepo kwenye kikosi klilichozima mzimu ulioisumbua klabu hiyo, Mwamnyeto alisema amefurahi kwa kutimiza ndoto na kuwapa raha mashabiki wa Yanga na kwamba kwa sasa wanaenda kujipanga ili kufanya vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita walipofika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika.

Mwamnyeto, aliliambia Mwanaspoti ni jambo kubwa na la kujivunia kwa kila mchezaji aliyeshiriki kufikia hatua hiyo kwa kuwa katika historia ataendelea kukumbukwa kwa mchango mkubwa walioutoa klabuni.

“Nimefurahi sana kila mchezaji katika mchezo alikuwa na hamu ya kuona timu inasonga mbele na kwa jitihada na uwezo wa Mungu tumefanikiwa,” alisema beki huyo wa kati aliyewahi kukipiga Coastal Union na kuongeza;

“Huko tunakoenda ndio kugumu zaidi, ila tutapambana tutafika mbali na kuiwakilisha nchi vizuri maana ni jukumu letu kama wachezaji kupambana kupata matokeo, hatua ya makundi sio mchezo maana timu zote zinakuwa bora.”

Mwamnyeto alisema awamu iliyopita walipoondolewa mapema Ligi ya Mabingwa Afrika na kushindwa kufikia malenmgo ya kutinga makundi, waliamua kukomaa kwenye Kombe la Shirikisho la kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kucheza fainali ya Shirikisho tangu michuano ilipoasisiwa 2004.

“Tulivyoteleza mwaka jana viongozi waliona upungufu uko wapi na sisi wachezaji tulipambana tukashindwa kufikia hatua hii Ligi ya Mabingwa msimu huu tukakubaliana tupambane kweli kweli na Mungu kasikia dua zetu,” alisema nahodha huyo aliyewapongeza mashabiki wa Yanga ambao muda wote wamekuwa karibu na timu yao iwe nyakati ngumu na hata zenye furaha hivyo waendelee kuwasapti maana nguvu yao ni kubwa katika kupata mafanikio hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: