Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto: Nahodha mwenye zari la makombe

Mwamnyeto Zmsh Mwamnyeto: Nahodha mwenye zari la makombe

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu wa 2023/24 nahodha Bakari Mwamnyeto alikuwa kiongozi wakitwaa taji la NBC, CRDB na katika Ligi ya Mabingwa Afrika wamegotea hatua ya robo fainali.

Mbali na makombe anaingia kwenye orodha ya nahodha aliyevaa medali ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya Yanga kuwa washindi wa pili.

Nyota huyo ameweka wazi kuwa wanatambua mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo jambo ambalo linafanyiwa kazi kila wakati na timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wote na benchi la ufundi.

Ni Miguel Gamondi anainoa Yanga iliyopata ushindi mbele ya Kaizer Chiefs ambayo inafundishwa na Nasreddine Nabi ambaye aliwahi kuifundisha Yanga na zama zake pia nahodha alikuwa ni Mwamnyeto.

Katika maandalizi kuelekea 2024/25 Yanga wametwaa Toyota Cup 2024 kwa ushindi wa mabao 4-0 Kaizer Chiefs ilikuwa ni Julai 28 2024 Yanga ilipata ushindi huo watupiaji wakiwa ni Prince Dube, Aziz Ki alitupia mabao mawili na Clement Mzize alitupia bao moja.

Nahodha huyo amesema: “Kwenye mechi ambazo tunacheza tumekuwa tukishirikiana na kikubwa ni kuona kwamba timu inapata ushindi hilo lipo wazi lakini muhimu ni kuona kwamba matokeo yanapatikana. Kwenye upande wa kunyua makwapa kila mmoja anapenda jambo ambalo linafanya tunashirikiana kila wakati.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: