Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto: Huu ni ubingwa wa Mashabiki

Mwamnyetoo Znd Mwamnyeto: Huu ni ubingwa wa Mashabiki

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati na nahodha wa Klabu ya Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto amesema kuwa Ubingwa wa 30 wa Ligi Kuu msimu huu ni maalum kwa ajili ya mashabiki zao ambao wamekuwa wakiwapa sapoti kila sehemu wanapokwenda kupambana.

Mwamnyeto amesema hayo baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya 30 baada ya kuitungua Mtibwa Sugar mabao 3-1 katika Dimba na Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

“Walichoka Wananchi msimu huu tumewapa tena, tunsshukuru kwa sapoti yao mwanzo mpa amwisho wa ligi, bado tuna mechi tatu lakini hapa tumeshamaliza kazi, tumekuwa mabingwa mara 30. Kwa heshima ya mashabiki na heshima ya uongozi, kombe hili ni la mashabiki.

“Siri ya kufanya vizuri ilikuwa ni kujitoa na kumsikiliza mwalimu, kila mechi ilikuwa kama fainali na mpaka sasa tunataka alama tatu kila mechi mpaka tunamaliza ligi. Mashabiki wamekuwa wakitoka mbali kuja kutupa hamasa, tulikuwa na deni kubwa la kuwalipa.

“Sisi ndio wachezaji wao, sisi ndio jeshi lao na sisi ndiyo timu yao, kazi yetu ni kuwapa alama tatu ili wafurahi na waweze kuridhika na kufurahi. Kwa hiyo tunasema kombe hili sio la wachezaji wala uongozi, hili ni kombe la mashabiki msimu huu,” amesema Mwamnyeto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live