Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamnyeto Foundation yatoa msaada vituo vya Watoto Yatima

Mwamnyeto Foundation Mwamnyeto Foundation yatoa msaad vituo vya Watoto Yatima

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamnyeto Foundation inayosimamia na nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto pamoja na kiungo wa timu hiyo Zawadi Mauya imetoa msaada katika vituo viwili vya watoto yatima ambavyo ni Mihayo na Mgolole vilivyopo mkoani Morogoro .

Juzi timu ya Mwamnyeto Foundation ilicheza na Timu ya Moro Combine katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kufungwa kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo.

Fedha zilizopatikana katika mchezo huo ndizo zimetumika kununulia mahitaji ya kusaidia katika vituo hivyo viwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live