Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambusi kutembeza panga Ihefu

Ihefu Mpunga Mwambusi kutembeza panga Ihefu

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Ihefu ikilia ratiba kuwa ngumu hali inayosababisha matokeo kutokuwa mazuri, Kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi amesema anaenda kufumua kikosi na kukisuka upya ili wanapoanza mzunguko wa pili watoke nafasi za chini.

Ihefu haijawa na matokeo mazuri licha ya kuwa timu pekee iliyoweka rekodi ya kuwafunga Yanga kwa mara ya kwanza baada ya kucheza mechi 49 bila kupoteza.

Timu hiyo ya mkoani hapa kwa sasa ipo nafasi ya 14 na pointi 11 na juzi ilikamilisha mechi za raundi ya kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Kabla ya mechi dhidi ya Kagera Sugar, Ihefu ilikuwa ugenini dhidi ya Geita Gold huko Nyankumbu, mjini Geita walipolala bao 1-0 kisha kurudi Mbarali Mbeya kuwavaa Yanga na kushinda 2-1 na sasa watawafuata Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini Pwani.

Mwambusi alisema ratiba si rafiki sana kwao, hali iliyowapa wakati mgumu vijana wake na kushindwa kupata matokeo mazuri akiahidi wanaenda kujipanga upya na mechi ya mzunguko wa pili dhidi ya Ruvu Shooting.

Alisema kwa muda aliokaa na timu kwa takribani mechi tisa, ameona upungufu katika baadhi ya maeneo anayopaswa kuyaongezea nguvu na kikao cha leo Jumatatu atawasilisha mapendekezo.

“Tunaenda kujipanga na mzunguko wa pili na keshokutwa Jumatatu (leo) tutakuwa na kikao kujadili maboresho kikosini kujua wangapi tuongeze na kuacha au kutoa kwa mkopo,” alisema Mwambusi. Kocha huyo wa zamani wa Mbeya City na Yanga, aliongeza, licha ya matokeo waliyonayo lakini raundi ya pili watarejea kibabe kuhakikisha wanafanya kweli na kubaki ligi kuu.

Chanzo: Mwanaspoti