Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambusi arejea Yanga

0d6f4c188a71101808fa0b85dbcd69a0 Mwambusi arejea Yanga

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UONGOZI wa Yanga umemrejesha kocha Juma Mwanbusi kama kocha wa muda wakati klabu hiyo ikitafuta kocha mwingine.

Januari 21 mwaka huu Mwambusi aliyekuwa chini ya Cedrick Kaze aliomba kupumzika katika nafasi yake ya ukocha kwa sababu za kiafya.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Yanga Dk. Mshindo Msolla alithibitisha kuwa Mwambusi anarejea kwenye klabu hiyo kama kocha wa muda wakati wakiendelea kutafuta mbadala wa Kaze aliyetupigwa virago mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Tunategemea Mwambusi ataichukua timu wakati tunatafuta kocha mkuu, bahati nzuri yeye aliondoka vizuri, amepata matibabu klabu imemsaidia kwenye matibabu yake amepata nafuu.”

“Hana ugeni wa timu tulikuwa naye hadi kwenye Kombe la Mapinduzi kwa hiyo kurudi kwake siyo jambo geni wakati tukiendelea na taratibu nyingine za kumpata kocha mkuu,” alisema Dk. Msolla.

Alisema makocha watatuma wasifu wao na kupelekwa kamati ya ufundi ili kupitia na kuona yupi anafaa kwenye klabu kwa sasa.

Mwambusi alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akiwa kama kocha msaidizi wa Zlatko Krimpotic ambaye baadaye alifutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Cedric Kaze.

Kabla ya hapo, kocha huyo aliyewahi kufundisha Mbeya City keshakuwa kocha msaidizi wa Yanga takriban mara tatu kwa nyakati tofauti.

Akiwa na kikosi cha Yanga msimu huu Mwambusi alihudumu kama kocha msaidizi kwenye michezo 18 ya ligi na kushinda michezo 13 huku wakitoa sare michezo mitano.

Yanga hivi karibuni ilivunja benchi la ufundi lililokuwa likongozwa na kocha Kaze ambaye amehudumu kwenye timu hiyo kwa siku 142 na kutwaa Kombe la Mapinduzi na kuicha Yanga ikiongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 45.

Wengine waliotemwa ni aliyekuwa msaidizi wa Kaze Nizar Khalfan, kocha wa viungo Edem Mortoisi, kocha wa makipa Vladmir Niyonkuru na ofisa usalama wa klabu Mussa Mahundi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz