Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambusi aliamsha Yanga

Mwambusi Pic Data.png Mwambusi aliamsha Yanga

Tue, 16 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author MABOSI wa Yanga wapo katika hatua ya mwisho ya kufanya uamuzi wa kupitisha jina moja la kuwa kocha mkuu wa timu yao, lakini jana kikosi chao kilirejea kambini ili leo kianze kujifua chini ya Kocha Juma Mwambusi anayekaimu nafasi ya Cedric Kaze aliyetimuliwa Jangwani.

Nyota wa Yanga walipewa mapumziko ya siku mbili tangu Ijumaa iliyopita na kutakiwa kuripoti jana ili kuanza kujifua kujiandaa na mechi yao ya Kombe la ASFC dhidi ya Tanzania Prisons na ile ya Ligi Kuu Bara watakapovaana na KMC mapema mwezi ujao.

Mabosi wa Yanga walitaka wachezaji hao warejee Avic Town jana saa 1:00 usiku ili wapate mlo wa pamoja na wajadiliane kwa kina na Mwambusi kabla ya leo kuamkia kwenye programu za kocha huyo aliyejiondoa kwa muda Jangwani ili kujiuguza kabla ya kurejea baada ya Kaze kutimuliwa.

Lakini kuitwa huko fasta kwa wachezaji kunatokana na mabosi kutofurahishwa na mwenendo wa timu hivyo wakiona ni bora wachezaji hao waendelee kusalia kambini ili waendelee kuwa fiti wakati wakimsubiri kocha mpya anayetarajiwa kutangazwa muda wowote kuanzia leo.

Mwambusi analiamsha kwa vijana wake leo asubuhi kuhakikisha kwamba wachezaji wa Yanga wanakuwa na utimamu wa mwili pamoja na pumzi ya kutosha ili akija kocha mkuu aendelee na programu nyingine.

Licha ya kwamba timu nyingi zimewapa mapumziko wachezaji wake kupisha likizo fupi ya timu ya Taifa Stars ambayo ina mchezo wa kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Equatorial Guinea utakaopigwa Machi 25, Yanga wao wanaendelea kujifua ili kujiweka sawa baada ya kuyumba katika duru la pili.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz