Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambusi: Simba, Yanga waiige Ihefu watatoboa Kimataifa

Mwambusi Juma Kocha Juma Mwambusi

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga Juma Mwambusi ameweka wazi kuwa klabu za Simba na Yanga zinauwezo wa kuzifunga Mamelodi na Al Ahly kwenye michezo yake ya kimataifa inayofuata mwishoni mwa wiki ijayo.

Mwambusi ametolea mfano namna ambavyo aliweza kuifunga Yanga iliyokuwa kwenye ubora wake ikifundishwa na Nabi yeye akiwa anainoa Ihefu kwa kipindi hicho.

Mwambusi amewaambia kuwa wanachotakiwa kukifanya ni kuheshimu ubora wa mpinzani, kuwajenga wachezaji kisaikolojia, kuiandaa timu kuwa timamu.

Pia Mwambusi ameeleza kuwa klabu hizo zinapaswa kuwanyima uhuru wachezaji wa timu pinzani wawapo uwanjani na mwisho amewataka kuzitumia nafasi wanazopata kwani huwa sio nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live