Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambusi, Ihefu waiwazia Simba

Juma Mwambusi Ihefu FC Kocha Juma Mwambusi

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Juma Mwambusi ameanza kuingiwa na wasiwasi wakati kikosi chake kitakapokabiliana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza jijini hapa, Mwambusi alisema mchezo huo ni mgumu kwao kutokana na ubora wa wapinzani wao pia kuwakosa wachezaji wake muhimu hususani mfungaji wake bora Jaffary Kibaya.

“Ni bahati mbaya kwetu kumkosa Kibaya kwa sababu wakati tuko kambini alipata taarifa za kuondokewa na mtoto wake hivyo tutapambana kadri ya uwezo wetu na wengine ambao wako kikosini,” alisema na kuongeza;

“Tunatarajia mchezo mgumu sana lakini kwa nafasi ambayo tupo tunapaswa kujiandaa vyema kuanzia kwenye aina ya uzuiaji wetu na wakati huo huo tukipambana kutafuta mabao yatayotuweka sehemu nzuri.” alisema.

Kwa upande wa kiungo wa timu hiyo, Papy Tshishimbi alisema kila mchezo kwao wanauchukulia kwa umuhimu mkubwa kwani kikosi walichonacho kina uwezo wa kupata matokeo chanya bila kujali mpinzani wanayecheza naye.

Katika kikosi hicho,Jaffar ndiye kinara wa kufunga mabao ambapo hadi sasa amefunga matatu huku mbali na yeye kukosekana ila pia itamkosa beki wake, Juma Nyosso anayetumikia adhabu ya kupewa kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo waliofungwa bao 1-0 na Azam FC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Oktoba 31.

Kwenye michezo tisa iliyocheza timu hiyo imeshinda mmoja tu, sare miwili na kupoteza sita ikiwa mkiani na pointi tano.

Chanzo: Mwanaspoti