Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba yuko fiti bana

Aucho 4989890 Khalid Aucho

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki qalisubiri sana kuona Picha ya namna hii ikipostiwa kwenye ukurasa wa Yanga SC, yes hii ndio picha ghari zaidi kwa kipindi hiki ambacho kinasubiriwa na wanayanga.

Picha ya Khalid Aucho 'Tank' kwangu ndio picha yenye kueleza namna ambavyo Yanga SC inaweza kufanya jambo pale nchini Afrika Kusini. Alikosekana mchezo wa mkondo wa kwanza, mkondo wa Pili uhitaji wake ni mkubwa zaidi.

Makoena wa Mamelodi Sundowns game ya kwanza aliutawala sana mchezo akaifanya timu ya Yanga SC muda mwingi wa mchezo wachezaji wasome zaidi namba za soli za viatu, hakukua na njia zaidi ya kulipaki kisha kushambulia Kwa kustukiza.

Aucho, Daktari anarejea kwenye eneo lake kwenda kutibu yale yote ambayo yalikuwa ni changamoto kwenye ule mchezo wa pale kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, naamini alikaa nje akisoma namna gani ya kuwafanya wakina Makoena kuwa bize kukaba/kulinda ili wasiruhusu bao la ugenini, yes Kwa Khalid Aucho huo uwezo upo tena ni mkubwa.

Dua zimefanya kazi watu wa Yanga SC siyo tu Kwa Khalid, pekee mwingine ambaye anahitajika kuwa fiti ni Pacome Zouzoua na Yao Yao, naweza kusema kama ikiwa hivyo Yanga SC inaenda kuishangaza Afrika pale Kusini mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live